Washirika
Welcome
Login

Ujaribiwapo, sifanye dhambi

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #64

   Umwombapo yu papo
   Akuongeze nguvu,
   Atakusaidia;
   Yesu atakufaa. 
 1. Ujaribiwapo, sifanye dhambi,
  Bali uzishinde, kwa Yesu kutii.
  Fuliza kiume ushinde tamaa;
  Yesu ni Mwokozi, hukuokoa.
 2. Wepushe waovu, matusi dharau;
  Heshima la Mungu, kamwe sisahau;
  Fanya uhodari, uwe mpole,
  Atakuokoa hata milele.
 3. Avumiliaye hupewa taji;
  Tujaposumbuka tu washindaji,
  Na mwokozi wetu hutuwezesha
  Tusiwe kushindwa kama twakesha.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Deni Ya Dhambi ilimalizika
  Tenzi #87 Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa. Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa. Kwake msalabani Nil...
 • Sioshwi dhambi zangu
  Tenzi:: #78 Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu. Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hap...
 • Naweka dhambi zangu
  Tenzi:: #48 Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni dam...

Submit Worship Music

RSS