Washirika
Welcome
Login

Twasoma, ni njema sana

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #104

 1. Twasoma, ni njema sana
  Mbinguni, kwa Bwana;
  Twasoma, dhambi hapana,
  Mbinguni kwa Bwana;
  Malaika wema wako,
  Vinanda vizuri viko,
  Na majumba tele yako,
  Mbinguni kwa Bwana.
 2. Siku zote ni mchana,
  Ni nchi ya raha;
  Wala machozi hapana,
  Ni nchi ya raha;
  Walioko wanuona
  Uso wa Mwokozi, tena
  Jua jingine hapana,
  Ni nchi ya raha.
 3. Nyama na vitu viovu
  Havimo kabisa;
  Kifo nacho, na ubovu,
  Havimo kabisa.
  Ni watakatifu wote,
  Wameoshwa dhambi zote;
  Wasiosafiwa wote
  Hawamo kabisa.
 4. Tuna dhambi, pia sote,
  Mwokozi akafa;
  Kwake tutaoshwa zote,
  Mwokozi akafa;
  Kwake twapata wokovu,
  Tutawona utukufu;
  Mbinguni tutamsifu;
  Mwokozi akafa.
 5. Baba, mama, ndugu zetu,
  Twendeni kwa Bwana;
  Huku chini sio kwetu,
  Twendeni kwa Bwana;
  Tusishikwe na dunia,
  Na dhambi kutulemea;
  Tutupe vya chini pia,
  Twendeni kwa Bwana.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Juu yake langu shaka
  Tenzi:: #134 Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu. Juu yake langu shaka, Yesu namuwekea...
 • Mapenzi ya milele
  Tenzi:: #135 Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwang...
 • Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi
  Tenzi:: #136 Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu, Sujuduni,malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu. ...
 • Yesu Mponya
  Tenzi:: #137 Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge Yesu ndiye mganga wetu Aponya wago...

Submit Worship Music

RSS