Washirika
Welcome
Login

Tazameni huyo ndiye

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #97

 1. Tazameni huyo ndiye,
  Mwenye kushinda vita;
  Haya, tumsujudie;
  Nyara anazileta;
  Watu wote msifuni,
  Sasa yumo kitini.
 2. Msifuni malaika,
  Mtukuzeni sana,
  Wote waliookoka
  Watamsifu Bwana;
  Watu wote msifuni,
  Sasa yumo kitini.
 3. Walimfanya dhihaka
  Zamani wenye shari,
  Kwao waliookoka
  Ni Bwana wa fahari;
  Watu wote msifuni.
  Sasa yumo Kitini.
 4. Nyimbo nzuri, sikizeni,
  Ni nyimbo za sifa kuu,
  Za Bwana Yesu kitini,
  Kutawazwa, yeye tu;
  Watu wote msifuni
  Sasa yumo Kitini.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi
  Tenzi:: #136 Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu, Sujuduni,malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu. ...
 • Huyo ndiye! anaskuka
  Tenzi:: #98 Huyo ndiye! anaskuka, Aliyetufilia, Wengi waliookoka, Wakimfurahia, Aleluya! Yesu aturudia. Sote tutamtazama, ...
 • Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu
  Tenzi:: #45 Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi. Mtazame Huyo! Aliyeangikwa j...

Submit Worship Music

RSS