Washirika
Welcome
Login

Siku ya Mbinguni kujawa na sifa

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #94

   Alinipenda, alinifia,
  Ameondoa na dhambi zangu;
  Alifufuka nipewe haki,
  Yuaja tena Mwokozi wangu.
 1. Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
  Dhambi zilizidi duniani;
  Yesu akaja azaliwe mtu,
  Awe na watu ulimwenguni.
 2. Na siku moja walikwenda naye,
  Wakamkaza msalabani;
  Aliumia, aliaibishwa,
  Ili atuokoe dhambini.
 3. Siku hiyo wakamlaza chini
  Kaburini alipumzika;
  Matumaini yetu wenye dhambi,
  Ni mwokozi, kwake twaokoka.
 4. Kaburi likashindwa kumshika;
  Jiwe likatoka mlangoni,
  Alifufuka kwa kushinda kwake,
  Naye yuko milele Mbinguni.
 5. Siku moja atatujia tena;
  Utukufu wake tutaona;
  Atawaleta na wapenzi wetu;
  Mwokozi: wangu, tutaonana.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Ewe, Baba wa Mbinguni
  Tenzi:: #107 Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombal...
 • Ni siku kuu siku ile
  Tenzi:: #56 Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Y...
 • Nipe Moyo Wenye Sifa
  Tenzi:: #55 Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi. Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ...

Submit Worship Music

RSS