Washirika
Welcome
Login

Peleleza Ndani Yangu

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi #59


Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
 1. Peleleza ndani yangu,
  Iwe safi nia,
  Kwangu kama kwako Mungu,
  Idhihiri pia.
 2. Peleleza moyo wangu
  Uunifunulie,
  Yaliyomo ndani yangu
  Nami niyajue.
 3. Kwanza washe zako tambi,
  Kumefunga giza;
  Nijue ambavyo dhambi
  Ni la kuchukiza.
 4. Peleleza na mawazo
  Ni mbegu za mambo,
  Asili ya machukizo,
  Maumbuo – umbo.
 5. Zidi kuyapeleleza
  Katikati yangu
  Hata wishe nifundisha
  Udhaifu wangu.
 6. Hapo nikikwinamia
  Mbele zako, Mungu,
  Hakika nitakujua
  U mpenzi wangu.
TOP Tenzi Trending
 

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Bwana u sehemu yangu
  Tenzi:: #116 Bwana u sehemu yangu, Rafiki yangu wewe; Katika safari yangu Tatembea na wewe; Pamoja na wewe, Pamoja na wewe...
 • Nilikupa Wewe Maisha Yangu
  Tenzi:: #112 Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nilikupa miaka Yangu d...
 • Kazi yangu ikiisha
  Tenzi:: #102 Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari. Kazi yangu ikiisha, nam...

Submit Worship Music

RSS