Washirika
Welcome
Login

Njoni enyi wa imani

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #76

 1. Njoni na furaha, enyi wa imani,
  Njoni Bethilehemu upesi !
  Amezaliwa jumbe wa Mbinguni;
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.
 2. Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga,
  Amekuwa radhi kuzaliwa;
  Mungu wa kweli, wala si kiumbe;
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.
 3. Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu,
  Mbingu zote na zijae sifa;
  Sifuni Mungu aliye Mbinguni;
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.
 4. Ewe Bwana mwema, twakubarikia,
  Yesu, utukufu uwe wako;
  Neno la Baba limekuwa mwili;
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Enyi wanadamu
  Tenzi:: #120 Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na mchunga? Yuko mchunga mmoja Mwenye ma...
 • Njoni Wenye Dhambi
  Tenzi:: #34 Njoni! Njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu awangojea ndiye awapendaye; Ajuaye awezaye kuwaponya ni Yeye...
 • Yesu Kwa iMani
  Tenzi:: #14 Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo. Nipe nguvu pia ...

Submit Worship Music

RSS