Washirika
Welcome
Login

Nilikupa Wewe Maisha Yangu

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #112

 1. Nilikupa wewe
  Damu ya moyoni,
  Ili wokolewe,
  Winuke ufuni:
  Nimekunyimani?
  Umenipa nini?
 2. Nilikupa miaka
  Yangu duniani
  Upate inuka,
  Kuishi Mbinguni:
  Nimekunyimani?
  Umenipa nini:
 3. Niliacha nuru
  Za Baba, Mbinguni,
  Kwingia taabu
  Za ulimwenguni:
  Nimekunyimani?
  Umenipa nini?
 4. Niliteswa sana,
  Mateso kifoni,
  Usije yaona
  Hayo ya motoni:
  Nimekunyimani?
  Umenipa nini?
 5. Nimekuletea
  Huku duniani
  Upendo na afya
  Zatoka Mbinguni:
  Nimekunyimani?
  Umenipa nini?
 6. Nipe siku zako,
  Udumu mwangani;
  Na taabu yako,
  Wingie rahani
  Nafsi, pendo, mali,
  Twae Imanweli.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Karibu na wewe
  Tenzi:: #129 Karibu na wewe, Mungu wangu Karibu zaidi, Bwana wangu Siku zote niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu...
 • Bwana u sehemu yangu
  Tenzi:: #116 Bwana u sehemu yangu, Rafiki yangu wewe; Katika safari yangu Tatembea na wewe; Pamoja na wewe, Pamoja na wewe...
 • Kazi yangu ikiisha
  Tenzi:: #102 Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari. Kazi yangu ikiisha, nam...

Submit Worship Music

RSS