Washirika
Welcome
Login

Ni Mfalme wa mapenzi

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #113

 1. Ni Mfalme wa mapenzi
  Ndiye anichungaye,
  Sipungukiwi, hawezi.
  Kunipoteza yeye.
 2. Kando ya mji mazima
  Yeye huniongoza
  Katika malisho mema
  Daima hunilaza.
 3. Mara nyingi hupotea
  Kwa ukaidi wangu,
  Naye huniandamia,
  Hunirudisha kwangu.
 4. Uvulini mwa mauti,
  Siachi hatari kamwe,
  Wewe Bwana huniachi,
  Mwokozi wangu wewe.
 5. Waniandikia meza
  Neema kwako tele.
  Kwa wewe, yote naweza.
  Na msalaba mbele.
 6. Kamwe hautapungua
  Uule wema wako;
  Mwisho, atanichukua,
  Juu, niimbe kwako.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Mapenzi ya milele
  Tenzi:: #135 Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwang...
 • Mapya ni mapenzi hayo
  Tenzi:: #110 Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa. Kila siku, Mapya pia Rehema, ...
 • Mapenzi yako yafanyike
  Tenzi:: #91 Mapenzi yako yafanyike, Wewe mfinyanzi, nami towe, Unifinyange upendavyo, Mimi tayari, naja kwako. Mapenzi yak...

Submit Worship Music

RSS