Washirika
Welcome
Login

Neno Lako Bwana

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #111

 1. Neno lako, Bwana,
  Ni imara sana;
  Lilo latwongoza,
  Lilo latufunza.
 2. Adui wabaya
  Wakikaribia,
  Neno lake Bwana
  Ni ulinzi sana.
 3. Siku za dhoruba
  Soma ukiomba;
  Neno lake Bwana
  Msaada sana.
 4. Ukiliamini,
  Hwenda na amani;
  Una na furaha
  Neno ni siraha.
 5. Ni furaha kweli,
  Na wingi wa mali,
  Neno lake Bwana
  Kwa wasiokana
 6. Neno la rehema,
  Tukali wazima;
  Faraja I papo,
  Tufarikanapo.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Niongoze, Bwana Mungu
  Tenzi:: #130 Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, nguvu sina: Nishike mkononi; U mkate wa Mbinguni, nilish...
 • Bwana Yesu Atakuja
  Tenzi:: #127 Bwana Yesu atakuja, Vumilia! Omba, ukiwa na haja, Vumilia! Mbingunu Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako, Nawe u...
 • Bwana Yesu
  Tenzi:: #122 Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, Mimi leo, naja kwako Ili niziungame. Bwana Ye...
 • Ni Ujumbe Wa Bwana
  Tenzi #118 Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama. Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya! w...

Submit Worship Music

RSS