Washirika
Welcome
Login

Ndiyo damu ya baraka

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #88

1. Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa,
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.

2.Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho,
Nami ni safi kabisa.

3.Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa;
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe kwa damu yako,
Nami ni safi kabisa.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

  • Si damu ya nyama
    Tenzi:: #119 Si damu ya nyama Iliyomwagika Iwezayo kuondoa Dhambi za wakosa. Yeye Bwana Yesu Sadaka ya Mungu, Mwenye damu ...
  • Damu imebubujika
    Tenzi:: #86 Damu imebubujika, Ni ya Imanweli, Wakioga wenye taka, Husafiwa kweli. Ilimpa kushukuru Mwivi mautini; Nami nis...
  • Ndiyo Dhamana Yesu Wangu
    Tenzi:: #19 Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye mwokozi wangu. Ndiyo dh...

Submit Worship Music

RSS