Washirika
Welcome
Login

Mwokozi Moyoni Mwangu

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #24

 Amani moyoni mwangu,
kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu yeye,
Yu nami moyoni mwangu.
 1. Tangu siku hiyo aliponijia,
  Akae moyoni mwangu,
  Sina giza tena, ila mwanga pia
  Kwa Yesu mwokozi wangu.
 2. Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
  Ndiye kiongozi wangu.
  Dhambi zangu zote zimeondolewa,
  Na Yesu, Mwanawe Mungu.
 3. Matumaini yangu ni ya hakika,
  Katika Mwokozi wangu.
  Hofu zangu na hamu zimeondoka,
  kwa kuwa ninaye Yesu.
 4. Siogopi tena, nikiitwa kufa,
  Yu nami daima, Yesu.
  Mlango wa Mbinguni ni yeye pia,
  “Tapita humo kwa damu.”
 5. Nitaketi na yeye huko milele,
  Nisifu Mwokozi wangu.
  Nina raha moyoni majira.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Mle kaburini Yesu Mwokozi!
  Tenzi:: #96 Bwana! Amefufuka, Kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, Sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu ha...
 • Msalabani Pa Mwokozi
  Tenzi #77 Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu. Msalabani pa mwokozi, Hapo niliomba upozi, Akan...
 • Ni Salama Rohoni Mwangu
  Tenzi:: #23 Salama rohoni,Ni salama rohoni mwangu. Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulis...

Submit Worship Music

RSS