Washirika
Welcome
Login

Mwenye dhambi huna raha

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #39

 1. Mwenye dhambi huna raha,
  Sikiza nakusihi,
  Utapata msamaha
  Kwake Yesu Mwokozi!
  Njoo hima, njoo hima,
  Naye atafurahi.
 2. Yesu anakwita sana
  Naye yuko Mbinguni;
  Hofu ya kifo hapana
  Kwake ukiamini.
  Njoo hima, njoo hima,
  Utapata amani.
 3. Hatakwita siku zote;
  Ni ya sasa nafasi.
  Lete na uchafu wote,
  Kukawa haipasi.
  Njoo hima, njoo hima,
  Ni wokovu halisi.
 4. .Uzima uko kwa Bwana
  Twae uzima hasa
  Bure unapatikana,
  Wokovu twae sasa!
  Njoo hima, njoo hima,
  Twae utakatifu.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Deni Ya Dhambi ilimalizika
  Tenzi #87 Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa. Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa. Kwake msalabani Nil...
 • Sioshwi dhambi zangu
  Tenzi:: #78 Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu. Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hap...
 • Ujaribiwapo, sifanye dhambi
  Tenzi:: #64 Umwombapo yu papo Akuongeze nguvu, Atakusaidia; Yesu atakufaa. Ujaribiwapo, sifanye dhambi, Bali uzishinde, kw...
 • Mwamba Mwenye iMara
  Tenzi #58 Mwamba wenye imara Kwako nitajificha! Maji hayo na damu Yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi. ...

Submit Worship Music

RSS