Washirika
Welcome
Login

Mungu msaada wetu

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #68

 1. Mungu msaada wetu
  Tangu myaka yote,
  Ndiwe tumaini letu
  La zamani zote.
 2. Kivuli cha kiti chako
  Ndiyo ngome yetu.
  Watosha mkono wako
  Ni ulinzi wetu.
 3. Kwanza havijakuwako
  Nchi na milima,
  Ndiwe Mungu; chini yako
  Twakaa salama.
 4. Na myaka elfu ni kama
  Siku moja kwako;
  Utanilinda daima
  Tu wenyeji wako.
 5. Binadamu huondoka,
  Mwisho hana kitu;
  Kama ndoto hutoweka
  Ndivyo hali yetu.
 6. Ila wewe Mungu wetu
  Ndiwe wa kudumu;
  Ndiwe bora, ngome yetu
  Twakaa dawamu.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Ni wako Mungu
  Tenzi:: #133 Aleluya enzi ndako; Aleluya,Amin. Aleluya,enzi ndako; Rejea Yesu. Ni wako Mungu! Ni furaha kwangu, Ni raha ku...
 • Niongoze, Bwana Mungu
  Tenzi:: #130 Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, nguvu sina: Nishike mkononi; U mkate wa Mbinguni, nilish...
 • Mungu ulisema
  Tenzi:: #124 Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru. Yesu ulik...
 • Bwana Mungu, nashangaa kabisa
  Tenzi:: #114 Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu. Bwana Mungu, na...

Submit Worship Music

RSS