Washirika
Welcome
Login

Mapya ni mapenzi hayo

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #110

 1. Mapya ni mapenzi hayo,
  Asubuhi tunayo,
  Saa za giza hulindwa
  Kwa uzima kuamshwa.
 2. Kila siku, Mapya pia
  Rehema, wema, na afya,
  Wokofu, na msamaha,
  Mawazo mema, furaha.
 3. Tukijitahidi leo
  Na mwendo utupasao,
  Mungu atatueleza
  Yatakayompendeza.
 4. Mambo yetu ya dunia
  Mungu atayang’aria,
  Matata atageuza
  Yawe kwetu ya Baraka.
 5. Yaliyo madogo, haya
  Mungu tukimfanyia,
  Yatosha: tutafaidi
  Huvuta kwake zaidi.
 6. Ewe Bwana, siku zote,
  Tusaidie kwa yote:
  Mwendo wetu wote vivyo,
  Uwe kama tuombavyo.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Mapenzi ya milele
  Tenzi:: #135 Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwang...
 • Ni Mfalme wa mapenzi
  Tenzi:: #113 Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye. Kando ya mji mazima Yeye hunion...
 • Mapenzi yako yafanyike
  Tenzi:: #91 Mapenzi yako yafanyike, Wewe mfinyanzi, nami towe, Unifinyange upendavyo, Mimi tayari, naja kwako. Mapenzi yak...

Submit Worship Music

RSS