Washirika
Welcome
Login

Mapenzi yako yafanyike

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #91

 1. Mapenzi yako yafanyike,
  Wewe mfinyanzi, nami towe,
  Unifinyange upendavyo,
  Mimi tayari, naja kwako.
 2. Mapenzi yako yafanyike,
  Unihoji dhambi zote,
  Unisafishe vya kimwili,
  Niinamapo Msalabani.
 3. Mapenzi yako yafanyike,
  Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
  Uwezo wote, kwako kweli,
  Sasa niponye, Ee, Mwokozi.
 4. Mapenzi yako yafanyike,
  Natoa kwako vitu vyote,
  Maisha, mali, moyo, mwili,
  Vyote ni vyako, kweli, kweli.
 5. Mapenzi yako yafanyike,
  Mapenzi yangu yavunjike,
  Ninakubali uwe Bwana,
  Ni mali yako, twaa kabisa.
 6. Mapenzi yako yafanyike,
  Unitawale siku zote,
  Sura ya Yesu umba kwangu,
  Nijaze Roho nayo nguvu.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Mapenzi ya milele
  Tenzi:: #135 Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwang...
 • Ni Mfalme wa mapenzi
  Tenzi:: #113 Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye. Kando ya mji mazima Yeye hunion...
 • Mapya ni mapenzi hayo
  Tenzi:: #110 Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa. Kila siku, Mapya pia Rehema, ...

Submit Worship Music

RSS