Washirika
Welcome
Login

Kazi yangu ikiisha

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #102

   Nitamjua, nitamjua,
nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua,
kwa alama za misumari.
 1. Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
  Na kuvaa kutokuharibika,
  Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni;
  Atakuwa wa kwanza kunilaki.
 2. Furaha nitapata nikiona makao
  Bwana aliyotuandalia;
  Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
  Vilivyonipa pahali Mbinguni.
 3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
  Nitawaona tena huko juu;
  Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
  Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
 4. Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
  Pasipo machozi wala huzuni.
  Nitauimba wimbo wa milele; lakini
  Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Bwana u sehemu yangu
  Tenzi:: #116 Bwana u sehemu yangu, Rafiki yangu wewe; Katika safari yangu Tatembea na wewe; Pamoja na wewe, Pamoja na wewe...
 • Nilikupa Wewe Maisha Yangu
  Tenzi:: #112 Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nilikupa miaka Yangu d...
 • Peleleza Ndani Yangu
  Tenzi #59 Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu. Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia, Kwangu kama...

Submit Worship Music

RSS