Washirika
Welcome
Login

Ewe, Baba wa Mbinguni

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #107

  
  Ee Mungu, bariki
  Ndugu hawa wawili!
  Ee Mungu, bariki
  Ndugu hawa wawili!
 1. Ewe, Baba wa Mbinguni,
  Usikie twombalo
  Hapa chini duniani,
  Na uwe radhi nalo
 2. Watu hawa mbele zako,
  Na mbele ya kanisa;
  Watimize Neno lako
  Wanakutana sasa.
 3. Kama Yesu na Kanisa,
  Ni mmoja, na hivyo,
  Watu hawawape sasa
  Wawe mmoja vivyo
 4. Walinde, Bwana, daima,
  Wabariki nyumbani
  Uwape nyingi salama
  Humu ulimwenguni.
 5. Wabariki, ewe Bwana,
  Watu hawa wawili,
  Wape upaji wa wana,
  Wafurahishwe kweli.
 6. Siku za duniani
  Zitakapopungua,
  Wape kurithi Mbinguni
  Mema ya kwendelea.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Siku ya Mbinguni kujawa na sifa
  Tenzi:: #94 Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu. Siku ya Mbing...
 • Baba yetu aliye Mbinguni
  Tenzi:: #29 Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi. Baba yetu aliye Mbinguni Amen...
 • Baba Mwana Roho
  Tenzi:: #6 Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Kila tukiamka tunakuabudu Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu,...

Submit Worship Music

RSS