Washirika
Welcome
Login

Deni Ya Dhambi ilimalizika

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi #87


Deni ya dhambi,
Msalabani,
Ilimalizikia,
Ni huru kabisa.
 1. Deni yangu ya dhambi,
  Yesu amelipa.
  Kwake msalabani
  Nilipewa uzima.
 2. Bwana Yesu asema,
  “Mwanangu dhaifu,
  Uwezo wa ushindi
  Hupatikana kwangu.”
 3. 3.Bwana, kweli naona,
  Nguvu zako pekee
  Huondoa ukoma,
  Niwe kipya kiumbe.
 4. Sina wema moyoni,
  Nidai neema,
  Nakubali kabisa,
  Kwa damu kusafiwa.
 5. Hata huko Mbinguni
  Miguuni pake,
  “Yesu alinifia,”
  Nitaimba milele.
TOP Tenzi Trending
 

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Sioshwi dhambi zangu
  Tenzi:: #78 Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu. Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hap...
 • Ujaribiwapo, sifanye dhambi
  Tenzi:: #64 Umwombapo yu papo Akuongeze nguvu, Atakusaidia; Yesu atakufaa. Ujaribiwapo, sifanye dhambi, Bali uzishinde, kw...
 • Naweka dhambi zangu
  Tenzi:: #48 Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni dam...

Submit Worship Music

RSS