Washirika
Welcome
Login

Baba yetu aliye Mbinguni

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16 | ወደ ቆላስይስ ሰዎች 3:16 | Col 3:16 | كولوسي 3:16 | Colosenses 3:16

Tenzi:: #29

 Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda, anipenda;
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda mimi.
 1. Baba yetu aliye Mbinguni
  Amenifurahisha yakini
  Kuniambia mwake chuoni
  Ya kuwa nami Yesu pendoni.
 2. Nimuachapo kutanga mbali,
  Yeye yu vivyo, hupenda kweli,
  Hunirejeza kwake moyoni;
  Kweli yu nami Yesu pendoni.
 3. Anipenda! Nami nampenda;
  Kwa wokovu alionitenda;
  Akanifia Msalabani
  Kwa kuwa nami Yesu pendoni.
 4. Haya kujua yanipa raha;
  Kumuamini kuna furaha;
  Humfukuza mara shetani,
  Kwona yu nami Yesu Pendoni.
 5. Sifa ni nyingi asifiwazo,
  Moja ni sana katika hizo,
  Wala siachi, hata Mbinguni,
  Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”.
Washirika

Post your comment

Comments

Be the first to comment

Related Articles

 • Ewe, Baba wa Mbinguni
  Tenzi:: #107 Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombal...
 • Siku ya Mbinguni kujawa na sifa
  Tenzi:: #94 Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu. Siku ya Mbing...
 • Anisikiaye aliye yote
  Tenzi:: #36 Ni “Atakaye”, ni “atakaye”, Pwani hata bara, na litangae; Ni Baba Mpenzi alinganaye At...

Submit Worship Music

RSS